Huduma
za usafiri wa ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta nchini Kenya zimesimamishwa kwa muda na hakuna anayeruhusiwa
kuingia katika uwanja huo kufuatia moto ilioliopuka majira ya asubuhi ya
leo katika moja ya majengo katika uwanja huo
Kwa
mujibu wa mkuu wa vipindi wa K 24 David Mbatia amesema chanzo cha moto
huo unaoendelea kudhibitiwa na vikosi vwa zimamoto bado hakijafahamika
japo kuwa hata hapo jana kumekuwa na kuchelewesha kuondoka kwa ndege
kadhaa
Aidha
mpaka sasa hakuna madhara kwa binadamu yaliyoripotiwa na kwamba jengo
linalodaiwa kuathiriwa ni katika eneo linalotumiwa na abiria kusubiria
muda na ndege zao.
No comments:
Post a Comment