Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya
kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari
wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki
iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.
Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu
ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa
ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi
zipuuzwe.Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.
Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tzTangazo hili limetolewa na: Mkurugenzi Mtendaji
No comments:
Post a Comment