NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua
Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini
Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai
kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake
wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.
Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa…
NI aibu sana! Ndivyo
unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad
Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana
na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya
ngono usiku kucha.
Katika
oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao
walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi
mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).
BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana,
aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako
baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.
Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni
ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote
kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.
ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo
alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo
ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume
wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’
aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.
BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa
ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo
mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini
akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.
MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na
mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na
kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde
asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia
makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za
matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa
kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa
wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.
MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri
kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya
hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.
INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa
zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu
katika ufukwe huo.
SOURCE:global publisher
No comments:
Post a Comment