Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha
mjini Mhe Godless Lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo
cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo
baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa
Kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus
Sabas alisema kuwa Mhe Lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira
ya saa 9 usiku.
Afande Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na
mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa
mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye
chombo hicho cha sheria.
Pia kamanda Sabas alisema kuwa Mh
Lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha
uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.
Kwa
upande mwengine Kamanda Sabas alisema kuwa zaidi ya hao watu 14 na Mhe.
Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa. Awali ilisemakana wakili
wake Albert Msando nae amekamatwa.
Mnamo siku ya Jumatatu
mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya Njiro jijini Arusha na watu
wasiojulikana hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta
vurugu chuoni hapo na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya.
Sekeseke
hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya
mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani
kuandamana.
No comments:
Post a Comment