http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Thursday, March 21, 2013

ligi ya mbuzi yaanza rasmi DUCE,,pata matokeo kamili hapa kwenye hii blog kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa ligi hiyo


Hile ligi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mpira wa miguu katika chuo kikuu cha elimu kishiriki  (DUCE) hatimaye yatimia,
Ilikuwa ni mishale ya saa ya saa kumi jioni pale michuano hiyo iliweza kufunguliwa na kiongozi wa wanafunzi chuoni hapo Mh. Fransisco Zebedayo.
Katika ufunguzi huo ulizikutnisha timu mbili ambazo ndio zilikuwa zinaonekana kuwa vibonde katika ligi hiyo nazo DARUSO pamoja na timu ya STAFF.
Mchezo huo wa ufunguzi ulianza rasmi mnamo mida ya saa kumi na nusu na kushuhudia sale pacha,lakini timu ya DARUSO inapaswa kujilaumu yenyewe kwa kukosa nafasi nyingi za wazi na umaridadi wa golikipa wa STAFF kwa kutoa michomo iliyokuwa hatari katika lango lake,
Ligi hiyo inatarajiwa kuendela mnamo hiyo kesho kwa kukutanisha
1st year Vs property market consults mnamo mida ya saa kumi kamili jioni katika viwanja vya chuo hicho (kiwanja kinapakana na Uwanja mpya wa taifa)


YAFUATAYO NI MATUKIO KATIKA PICHA

 Raisi wa wanafunzi na mwalimu wa michezo DUCE
wachezaji wote kwa pamoja kabla ya mpambano kuanza
                                              kikosi cha   DARUSO


                                                                  kabla ya mechi kuanza


 makocha wa kikosi cha DARUSO
 hawa ni baadhi ya mashabiki katika mechi hiyo ya ufunguzi
 huu ni wakati wa mapumziko
                                                     mashabiki wa timu ya DARUSO
                        Timu ya DARUSO ikijiandaa kwenda kumalizia kipindi cha pili
wachezaji wa timu ya staff wakiwa mapumzikoni kabla ya kipindi cha pili

No comments:

Post a Comment