Serikali ya Tanzania kupitia
kamati ya maadili ya Mamlaka ya Mawasiliano TCRA imevifungia kwa muda wa
miezi sita vituo vya radio ya Iman Morogoro na radio Kwa Neema Mwanza
kutokana na kukiuka kanuni na taratibu za utangazaji kinyume na sheria
namba 5 ya utangazaji ya mwaka 1993.
Makamu mwenyekiti wa hiyo
kamati Walter Bigonya amesema kwa time tofauti hivyo vituo vimekua
vikishiriki kurusha matangazo ya uchochezi kwa Watanzania ambapo Iman
wamedaiwa kushiriki kuhamasisha watu wasishiriki zoezi la sensa ya watu
na makazi wakati kituo cha redio cha kwa Neema kimeshiriki kueneza
uchochezi juu ya kuchinja kati ya Waislamu na Wakristo.
Kwenye hatua nyingine kamati
hiyo imekipiga faini ya shilingi milioni 5 kituo cha radio cha Clouds Fm
kutokana na kurusha matangazo yanayoashiria uhamasishaji wa vitendo vya
kishoga kupitia Power Breakfast january 23 2013 ambapo Mkurugenzi wa
utafiti na uzalishaji Ruge Mutahaba amesema uongozi umepanga kukata
rufaa kupinga hiyo adhabu ili kutoa nafasi zaidi ya kufanyika uchunguzi
wa hayo madai.
No comments:
Post a Comment