]
Isco akitambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia Real Madrid. |
Isco amepewa jezi namba 23 ambayo ilikuwa ikivaliwa na gwiji David Beckham |
Isco akisaini mkataba mbele ya Florentino Perez - Raisi wa Real Madrid |
Kwenye kabati la makombe |
OFFICIAL: FC TWENTE YAMKANA RASMI SHOMARI KAPOMBE.
RICHARD PETERS
KLABU
ya FC Twente ya Uholanzi usiku huu imemkana rasmi mchezaji wa Simba na
Taifa Stars, Shomari Kapombe ambaye alitangazwa kuwa na mipango ya
kujiunga na kalbu hiyo.
Kwa muda wa wiki mbili sasa, vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania
viliripoti taarifa za Kapombe kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi ambayo
ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi katika msimu wa 2009-10,
pia ilifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
katika msimu huo.
Afisa
Habari wa FC Twente, Richard Peters amekiambia kipindi cha michezo cha
redio Clouds FM usiku huu kwamba, klabu yaje haijawahi kumuhitaji
mchezaji huyo na hana taarifa zozote kuhusu Kapombe.
“Kwa sasa hatuhitaji mchezaji yeyote kutoka Afrika na hata kama ingekuwa hivyo ingefahamika. Nasisitiza hatuna mpango na mchezaji huyo,” amenukuliwa Peters akikataa kumtambua Kapombe.
Kwa
upande wa viongozi wa Simba mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed
Nkwabi alikaririwa na gazeti la Mwananchi hivi karibuni akisema kwamba,
“Timu atakayokwenda kufanya majaribio Kapombe huko nchini Uholanzi ni
FC Twente, suala la ataondoka lini kwenda kufanya majaribio tutawaambia
safari itakapokuwa tayari.”
Na kwa upande wa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden
Rage alikaririwa akizungumza kwenye kipindi cha michezo cha redio moja
hapa jijini, akisema kwamba amekwishatoa kibali kwa Kapombe kuondoka
nchini siku yoyote kuanzia sasa kwa ajili ya kufanya majaribio nchini
Uholanzi.
Lakini
baada ya kuwepo kwa taarifa hizi mtandao huu ulijaribu kufanya utafiti
kidogo kuhusu suala la usajili wa mchezaji huyu kwenda FC Twente na
kugundua vitu kadhaa vya utata kuhusu ukweli wa taarifa za Kapombe
kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi.
Miongoni
mwa vitu vya kushangaza ni mtandao uliotangazwa kuandika habari hizo
pia majibu ya wakala wa mchezaji huyo aitwaye Denis Kadito ambaye
alithibitisha ni ukweli kwamba alikuwa katika mpango wa kumpeleka
Kapombe Uholanzi ili aanze kumtafutia timu ndani ya bara la ulaya, na
alipoulizwa kuhusu taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente, Dennis
alisema hana taarifa zozote za Kapombe kutakiwa na FC Twente hivyo
hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.
USAJILI: KEVIN STROOTMAN AENDI POPOTE MSIMU HUU - ASEMA MKURUGENZI WA PSV
Mkurugenzi wa michezo wa PSV Marcel Brands ameweka wazi kwamba klabu yake haina mpango wowote wa kumuuza Kevin Strootman kuelekea msimu mpya wa 2013-14 .
Kiungo huyo wa kiholanzi kwa muda mrefu sasa amekuwa akihusishwa sana na uhamisho wa kwenda Manchester United, wakati klabu ya Napoli pia imeonyesha nia ya kumhitaji kiungo huyo mwenye miaka 23.
"Hatutaki kumuuza Strootman msimu huu. Anajua kwamba kwamba atabaki PSV kwa msimu mwingine," Brands aliiambia De Telegraaf.
Strootman ni zao la academy ya Sparta na pia alishawahi kuvaa jezi ya klabu ya Utrecht kabla ya kujiunga na PSV mwaka 2011. Tangu wakati huo ameimarika na kuwa mmoja wa viungo bora bora chipukizi barani ulaya.
Ana mkataba na PSV unaodumu mpaka mwaka June 2016.

SPURS WAKAMILISHA USAJILI PAULINHO - ADEBAYOR KUMPISHA SOLDADO WHITE HART LANE
Mshambuliaji Emmanuel Adebayor anaweza akawa njiani kuondoka White Hart Lane.
Tottenham Hotspur jana usiku ilikamilisha usajili wa kiungo wa kibrazil Paulinho kutoka Corinthians.Na sasa Andre Villas-Boas anahamishia akili yake katika ushambuliaji, huku mshambuliaji wa Valencia Roberto Soldado akiwa ndio chaguo lake la kwanza.
Boss huyo wa Spurs anategemea kumuuza Adebayor kwa klabu ya Besiktas ambayo ipo tayari kulipa kiasi cha £5m kwa ajili ya Mtogo huyo.
Dili hilo linaweza likamvutia zaidi Adebayor kutokana na kodi ndogo ya asilimia 15 wanayokatatwa wachezaji kwenye mishahara yao.
Adebayor, 29, ana mkataba wa miaka miwili na Spurs ambao unampatia kiasi cha £80,000 kwa wiki lakini anaonekana yupo njiani kuondoka.
Villas-Boas anataka kumuondoa mshambuliaji huyo wa Togo kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa ili amuongezea Soldado.
Tottenham wapo tayari kulipa kiasi cha £15m — lakini Valencia wanataka kiasi cha £25m.
Raisi wa Valencia Amadeo Salvo Lillo alisema: “Tumekuwa na matatizo mengi ya kifedha lakini hatuna ulazima wa kuanza kuuza wachezaji kwa bei zisizostahili”
EXCLUSIVE: UKWELI KUHUSU SHOMARI KAPOMBE KUTAKIWA NA FC TWENTE HUU HAPA!
Kwa wiki kadhaa zilizopita kumekuwepo na taarifa nyingi zinazomuhusu beki
wa kimataifa wa Tanzania na timu ya Simba, Shomari Kapombe kwamba
anatarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni kwenda nchini Uholanzi kwa
ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya FC Twente.
Kapombe
ambaye mwaka jana alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa Tanzania amekuwa
na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na Simba akitokea Polisi Morogoro
miaka mitatu iliyopita kwa kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Karibia
vyombo vya habari vyote nchini vimekuwa vikikaririwa kwamba Shomari
Kapombe anatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika klabu ya FC Twente,
ambayo ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uholanzi katika msimu wa 2009-10,
pia ilifanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
katika msimu huo.
Kwa upande wa viongozi wa Simba mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Swed Nkwabi alikaririwa na gazeti la Mwananchi akisema
kwamba,”timu atakayokwenda kufanya majaribio Kapombe huko nchini
Uholanzi ni FC Twente, suala la ataondoka lini kwenda kufanya majaribio
tutawaambia safari itakapokuwa tayari.”
Na kwa upande wa mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alikaririwa akizungumza kwenye kipindi cha michezo cha Spoti Leo cha
Radio One akisema kwamba amekwishatoa kibali kwa Kapombe kuondoka
nchini siku yoyote kuanzia sasa kwa ajili ya kufanya majaribio nchini
Uholanzi.
Lakini
baada ya kuwepo kwa taarifa hizi mtandao huu ulijaribu kufanya utafiti
kidogo kuhusu suala la usajili wa mchezaji huyu kwenda FC Twente na
kugundua vitu kadhaa vya utata kuhusu ukweli wa taarifa za Kapombe
kutakiwa na klabu hiyo ya Uholanzi.
UKWELI
Mtandao feki |
1:
Kwanza kabisa chanzo kikuu cha taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente
zilizotolewa na mtandao wa www.fctwente.nu - ambao sio mtandao rasmi wa
klabu ya FC Twente.
Kwa
mujibu wa mtandao rasmi wa klabu ya FC Twente anuani yake ni hii
(http://www.fctwente.nl/en/). Mtandao huu rasmi wa klabu hii haukuwa na
taarifa zozote kumuhusu Shomari Kapombe au mchezaji mwingine wa Simba na
Tanzania kiujumla.
2:
Katika kupata uhakika zaidi mtandao huu ulijaribu kuwasiliana na afisa
habari wa klabu ya FC Twente, Bwana Richard Peters kuhusu ukweli wa
klabu yake kumtaka Shomari Kapombe kutoka Tanzania. Lakini afisa habari
huyo alikanusha taarifa hizo na akisema kwamba klabu yake haina taarifa
zozote kuhusiana na mchezaji huyu Kapombe. Akisisitiza kwamba mtandao
ulioripoti taarifa za usajili wa Kapombe sio sahihi na zimetolewa na
mtandao usio rasmi.
3:
Mtandao huu haukuishia hapo, tulijaribu kumtafuta wakala
anayeshughulikia kumtafutia Kapombe timu nje ya Tanzania, Bwana Denis
Kadito ambaye alithibitisha ni ukweli kwamba alikuwa katika mpango wa
kumpeleka Kapombe Uholanzi ili aanze kumtafutia timu ndani ya bara la
ulaya, na alipoulizwa kuhusu taarifa za Kapombe kutakiwa na FC Twente,
Dennis alisema hana taarifa zozote za Kapombe kutakiwa na FC Twente
hivyo hawezi kutoa maoni yoyote kuhusu suala hilo.
NEYMAR KUFANYIWA UPASUAJI WA KOO IJUMAA HII KABLA YA KUJIUNGA NA
BARCELONA
Mchezaji bora wa mashindano ya kombe la mabara Neymar ambaye jana aliisadia timu yake kushinda ubingwa wa mabara kwa kuifunga Spain 3-0, amesema hatojiunga na klabu yake mpya ya Barcelona mpaka atakapofanyiwa upasuaji wa koo.
Neymar, ambaye amejiunga na Barcelona akitokea Santos kwa ada ya uhamisho wa 57 million euros jana alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kombe la mabara baada ya kupigiwa kura nyingi na waandishi wa habari na kukabidhiwa mpira wa dhahabu.
Mbrazili huyo mwenye miaka 21, ambaye alifunga mabao manne katika mashindano ya mabara, alikaririwa akisema kwamba atafanyiwa upasuaji siku ya Ijumaa kabla hajaenda Spain kujiunga na Barca.
"Ni tatizo ambalo ninalo, koo langu lina matatizo, hivyo itabidi nifanyiwe upasuaji ili kutatua tatizo hilo liishe kabisa," alisema Neymar huku akisisitiza ugonjwa wake huo siku mkubwa sana.

No comments:
Post a Comment