Kocha wa Chelsea Rafa Benitez anapigana historia leo hii na anaweza kuishinda ikiwa atapata matokeo chanya dhidi ya timu yenye mkosi na makocha wa Chelsea - West Bromwich Albion.
West Brom, ambao wanaenda Stamford Bridge leo jumamosi, wamekuwa moja ya vyanzo vikuu vya kuondolewa kwenye benchi la ufundi la Chelsea kwa makocha wawili waliopita wa klabu hiyo. Mwaka mmoja uliopita goli la Gareth McAuley liliipa ushindi West Brom, na kumfukuzisha kazi Andre Villas Boas.
Miezi nane baadae, ushindi wa 2-1 kwenye uwanja wa Stamford Bridge dhidi
ya Chelsea ukamaliza siku za kufundisha Chelsea kwa Robert Di Matteo.
Je leo Benitez atavunja mwiko na kuishinda historia dhidi ya West Brom?
No comments:
Post a Comment