Habari ambazo thehabari.com imezipata kutoka kwa
baadhi ya Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba
Mtanzania aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani
Japhari ameaga dunia kwa kujinyonga.
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo, alisema ” I
hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani
ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo
mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha
shughuli zote zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu“, alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya
kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea
kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara. Vijana wengi waliokuwa
wakifika Urusi ki masomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na
wengine kumtaka ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu
wake wa Mji.
Marehemu Shabani, ameacha mke na watoto Kandhaa, na dua zetu
tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia yake nyingine kubwa, iliyopo
Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na msiba huu, ambao bado
umetuacha na maswali mengi, bila majibu.
Thehabari.com itaendelea kuwafahamisha wadau maendeleo ya msiba huu kadri tutakavyokuwa tunapata taarifa.
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=34812
No comments:
Post a Comment