Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza
nafasi za kazi 1,134 katika sekta mbalimbali za ofisi za umma.
Kwa mujibu
wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi nafasi
hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ya
www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Katibu
alifafanua kuwa nafasi 949 ni kwa ajili ya waajiri walioainishwa katika ofisi
za wizara, halmashauri na nyingine 185 ni za taasisi na wakala mbalimbali za
Serikali.
Aidha,
amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya
kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya
Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao Aprili 9, 2013.
Daudi
alifafanua kuwa waajiri ambao watatoa ajira hizo ni makatibu wakuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa
Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Maendeleo Jinsia na
Watoto, Wizara ya Kazi na Ajira na Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo.
Wengine ni
Makatibu wakuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,
Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Wizara ya
Nishati na Madini, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Ardhi Nyumba
na Makazi, Wizara ya Maji na Katibu Ofisi ya Rais Maadili.
Wengine ni
Makatibu Tawala wa Mikoa ya Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga,
Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi,
Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha; pamoja na wakurugenzi wa halmashauri
za majiji na manispaa Mwanza, Iringa, Songea, Shinyanga, Morogoro, Singida,
Kigoma/ Ujiji na Temeke.
Nafasi
nyingine ni kwa ajili ya wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mufindi, Kyela,
Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro,
Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa
na Meatu.
Nyingine ni
Wilaya za Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto,
Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro, Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida,
Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro na Kiteto.
Pia zimo
Wilaya za Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa
na Tandahimba pamoja na halmashauri za miji ya Njombe na Kibaha. Nafasi
nyingine ni za Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) na Wakala wa Ufundi na
Umeme (Temesa).
Nafasi hizo
zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya
Kompyuta daraja la II – (nafasi 10), Ofisa Vipimo II – nafasi 6, Mpima Ardhi,
daraja la II (nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9,
Ofisa Mipango Miji daraja la II– nafasi 13 na Mhandisi daraja la II - Ujenzi
(Nafasi 16).
Pia
wanahitajika wahandisi daraja la II - Maji (Nafasi 13), Ofisa Misitu daraja la
II (nafasi 7), Ofisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu daraja la II –
nafasi 8 na nyingine mbalimbali.
No comments:
Post a Comment