Mheshimiwa Balozi Hamisi
Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka
Lichinga nchini Msumbiji waliofika katika maadhimisho hayo.
………………………………………………………………….
Maadhimisho ya Tamasha la
Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni Kitaifa yamekuwa
yakiadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Februari, Mkoani Ruvuma kuanzia
mwaka 2010. Dhana ya maadhimisho haya ni kufanya Kumbukizi za Vita ya
Majimaji ziwe kichocheo cha mabadiliko kwa jamii kifikra na
Kiutamaduni. Kuwaleta pamoja wadau wa historia ya Vita vya Majimaji
Pia kuwakumbuka Mashujaa wa
Vita vya Maji Maji walionyongwa tarehe 27 Februari,1906 na Wajerumani
ambao wamezikwa katika eneo la Makumbusho ya Kumbukizi ya Vita vya
Majimaji – Songea
Vilevile Kutoa fursa kwa jamii
kushiriki katika kuenzi na kuendeleza urithi wetu kupitia shughuli za
kimila zinazofanywa na Wazee wa Baraza la Mila na desturi za jamii
iliyohusika katika tukio la Vita vya Maji Maji.
Na kutoa elimu kwa Umma wa Watanzania kwa ujumla kuhusu Kumbukumbu za Kimakumbusho kupitia matukio ya kimila na kihistoria.
Kuweka dhahiri madhumuni ya kuanzishwa kwa Makumbusho ya Taifa nchini kwa vitendo.
Katika maadhimisho haya Waziri
wa Mali asili na utalii Dkt.Hamis Kagasheki ameitaka jamii nchini kuenzi
harakati hizo zilizofanywa na mababu wa taifa hili katika kupinga
utawala wakikoloni.
Pia amesema amefurahishwa kuona
kuwa maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya majimaji yamekuwa na historia
ya kuadhimishwa mwezi februari Mkoani Ruvuma katika ngazi ya mkoa tangu
nchi yetu ipate uhuru, Hii imelenga kuwakumbuka Mashijaa wa Vita vya
Maji Maji.
Hii imeonyesha kwa jinsi Uongozi
wa mkoa , Wazee wa Baraza la Mila na Desturi na wananchi wanavyothamini
mchango waliokuwa nao Mashujaa hawa hata kujitoa mhanga kutetea uhuru,
haki na utawala wao pamoja na kulinda mila , tamaduni na rasilimali
zilizopatikana kwenye maeneo yao kwa manufaa ya jamii na taifa kwa
ujumla.
Hili ni jambo la kuigwa na kila mtu kuthamini na kulinda urithi wetu wa utamaduni kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijazo.
Akiendelea kusema ameshuhudia
kuwepo kwa taarifa za mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama
Mkomanile ambaye alishiriki katika harakati hizo za mapambano dhidi ya
utawala wa kikoloni hivyo ni ishara kuwa akina mama nao walishiriki
kikamilifu katika mapambano hayo dhidi ya ukoloni ambapo kwa upande wa
Tanganyika ilikuwa ni Vita ya Maji maji ,na kwa upande wa Kenya ilikuwa
ni Mau mau na vyote vilikuwa ni chanzo cha vuguvugu la ukombozi wa bara
la Afrika.
Pia ametoa wito kwa wadau wa
utafiti kufanya utafiti zaidi habari za mwanamke huyo ili nazo ziweze
kuingizwa kwenye historia ya kumbukizi hiyo ya vita ya Maji Maji ambayo
pia ilikuwa ni chachu ya ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi.
Baadhi ya wazee wakiwa wameshika
Silaha za Jadi walizotumia mababu zetu kupigania dhidi ya kupinga
utawala wa Wakoloni wa Kijerumani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Kamanda wa Jeshi la wananchi akiweka upinde
Mpiganaji wa vita kuu ya pili ya Dunia
Mzee Komba akisindikizwa na kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
kwenda kuweka shahada ya uwa katika mnala wa mashujaa.
Hii ni kwa nje ndivyo hali ilivyokuwa
Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri
wa Maliasili na Utalii pamoja na viongozi wengine wakitoa salamu ya
heshima kwa mashujaa wa majimaji
Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezi kwa njia ya kijeshi
No comments:
Post a Comment