Na Boniface Wambura
TIMU
tatu zimeshuka daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kurudi
Ligi ya Mkoa msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kushika nafasi za mwisho
katika ligi hiyo msimu huu 2012/2013 iliyomalizika wikiendi iliyopita.
Small
Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada ya kuondolewa kwenye
michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye moja ya mechi
zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza yalifutwa.
Moro
United ya Dar es Salaam ndiyo iliyoaga FDL kutoka kundi B baada ya
kumaliza mechi zake ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi C timu
iliyoshuka ni Morani ya Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na
moja.
Timu
zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao
wa 2013/2014 ni Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A ikiwa na pointi
31, vinara wa kundi B timu ya Ashanti United ya Dar es Salaam yenye
pointi 29 wakati Rhino Rangers ya Tabora imepanda kutoka kundi C ikiwa
na pointi 32.
No comments:
Post a Comment