Na Boniface Wambura
WATAZAMAJI
13,398 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati
ya Yanga na Kagera Sugar lililochezwa juzi (Februari 27 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 77,117,000.
Mechi
hiyo namba 130 iliyochezeshwa na Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani
ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 42 kuibuka
na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 45 na Haruna Niyonzima.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 18,291,297.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 11,763,610.17.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 11,908 na kuingiza sh. 59,540,000 wakati idadi
ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 80 na kuingiza sh. 1,600,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,300,659.97,
tiketi sh. 3,348,990, gharama za mechi sh. 5,580,395.98, Kamati ya Ligi
sh. 5,580,395.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,790,197.99 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,170,153.99.
Wakati
huo huo: Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho kwa Polisi Morogoro
kuikaribisha Oljoro JKT ya Arusha kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Hata
hivyo, timu hizo haziko katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa
ambapo Yanga ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 wakati
Oljoro JKT inayofunzwa na Alex Mwamgaya ikiwa nazo 21 na Polisi Morogoro
pointi 15.
Oljoro
JKT iko katika nafasi ya tisa. Polisi Morogoro ambayo katika mzunguko
wa pili imebadilika ikiwa chini ya Kocha Adolf Rishard inashika nafasi
ya 12 ikiziacha mkiani Toto Africans yenye pointi 14 na African Lyon
ambayo ina pointi 13.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Machi 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Oljoro
JKT vs Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), African Lyon vs Ruvu
Shooting (Azam Complex, Chamazi) na Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar
(Mkwakwani) wakati Machi 7 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Kagera Sugar (Azam
Complex, Chamazi).
Machi
9, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Yanga vs Toto Africans Uwanja wa
Taifa), na Azam vs Polisi Morogoro (Azam Complex, Chamazi).
No comments:
Post a Comment