ROMAN
Abramovich ataangalia upya nafasi ya Rafa Benitez kama kocha wa muda wa
Chelsea, baada ya mashabiki konyesha kutokumtaka kocha huyo baada ya
mechi ya Jumamosi dhidi ya West Bromwich.
Benitez
amewakera mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuwaponda dakika chache
baada ya klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Middlesbrough na kujihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ya Kombe
la FA dhidi ya Manchester United.
Zaidi
ya mashabiki 1,900, waliojitolea kusafiri kwa umbali wa Mile 500 kwenda
kuishangilia timu yao walishangazwa na jinsi alivyowaponda, wakati wa
mechi hiyo dhidi ya vibonde wa Ligi Daraja la Kwanza, na sasa asubiri
kupata wakati mgumu dhidi ya Stamford Bridge.
Huruma:
Benitez akiiongoza timu yake mazoezini jana, amekuwa na wakati mgumu
kutoka kwa mashabiki tangu siku ya kwanza alivyofika kwenye klabu hiyo.
Abramovich
tayari anaangalia machaguo yake baada ya Benitez kuitwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Chelsea, Ron Gourlay kuzingumza juu ya matatizo ndani ya
klabu hiyo.
Mmiliki
wa klabu hiyo anakosa mtu muafaka atakayechukua majukumu ya kuinoa
Chelsea kwa muda, lakini Jose Mourinho, ambaye alitosa kurejea klabuni
hapo msimu uliopita na kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini wanafikiriwa
kuchukua jukumu hilo msimu ujao.
Klabu
hiyo imesema kwamba hata wazuia mashabiki kuendelea na mgomo wao dhidi
ya kocha huyo wa zamani wa Liverpool, hii imekuja baada ya wiki hii
kuwaandikia barua Chama cha mashabiki wa Chelsea.
Ruksa: Mashabiki hawatazuiwa kuingia na mabango yao ya kumpinga Benitez kesho
Ofisa
mmoja wa Chelsea alisema: “Napenda kuliweka hili bayana, klabu haina
utaratibu wa kuzuia au kukutaza watu kuingia na mabango, kinachokatazwa
ni mabaongo ya kutishia, matusi au ya kibaguzi au yatakayoziba wengine.
“Kwenye
miaka ya nyuma mashabiki wamekuwa wakiruhusiwa kuingia na mabango
ambayo waliyatumia kutoa dukuduku lao kuhusu klabu, na hatuna mpango wa
kuzuia hilo.”
Chelsea hawataangalia suala la usalama kwenye mechi ya Jumamosi, licha ya maneno yaliyotolewa na Benitez, dhidi ya mashabiki.
Alhamisi
alijaribu kumaliza bifu lake na mashabiki baada ya kukubali kufanya
mahojiano na mwandishi wa BBC, Dan Walker. Alivunja sera ya klabu ya
kuomba ruhusa kabla ya kufanya mahojiano na Chelsea hawakujua kama
Benitez pale alipopanda gari baada ya mazoezi. Mahojiano hayo yatarushwa
kwenye kipindi cha Football Focus, kesho.
Kwenye
kipindi hiki Benitezi alisema: “Kila mtu anajua ni muhimu kamaliza
kwenye timu nne za juu, au tatu, ilikuwa na uhakika wa kushiriki Ligi ya
Mabingwa msimu ujao. Nataka kushinda kila mechi. Hivyo naweza kusema
njia pekee ya kuibeba timu ni kuwaunga mkono wachezaji. Kama mashabiki
wataendelea kuimba nyimbo za kuiponda timu – tulikuwa tnaongoza kwa
mabao 2-0 lakini waliengelea kutuponda, sidhani kama watatushangilia
tukiwa nyumbani.
“Uhusiano
wangu na watu ndani ya klabu ni mzuri, uhusiano wangu na mmiliki ni
mzuri na kila mara huwa naongea na Abramovich kuhusu soka, nafurahia
sana. Sina tatizo na mtu.
Akifunguka: Benitez akizungumza na mwandishi wa BBC, Dan Walker, jana
Benitez
alipewa jukumu la kuisaidia timu kumaliza kati ya timu nne za juu baada
ya kuchukua mikoba ya Roberto Di Matteo, Novemba, mwaka jana.
Di
Matteo alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kushinda michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu uliopitia, lakini Benitez amesisitiza kwamba yeye
anauzoefu unaombeba. Aliongeza: “Nilipokuja, tulikuwa tunakaribia
kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, walitakiwa kufanya kitu na
wakaamua kuwa mimi nina uzoefu nitafanya vizuri na nikaanza kazi yangu.
“Mwanzo
ilikuwa ngumu kwa sababu kulikuwa na mechi moja kila baada ya siku tatu
na baadaye ikawa rahisi kwa sababu wachezaji ni wazuri sana wanafanya
mazoezi vizuri hata na hali ya hewa ndani ya klabu.”
Champion of Europe: Roberto Di Matteo retains huge support at Chelsea
‘It was difficult at the beginning
because it was one game each three days, and after it was easier because
you could see the players are really good, they train really well, they
are keen to learn, so the atmosphere in the club is good.
When asked if he would be sacked, he replied: 'No. They know how we work and what we are trying to do.'
He added: 'The players are really happy in what we are trying to do. Sometimes you win, sometimes you cannot.
'There are no issues in the team. In terms of what we do, the players are fully behind the methods.
'If we stick together and support the
players, we will be able to win games. Then at the end of the season I
will leave and then they can criticise.'
No comments:
Post a Comment