Huyu ni mmoja wa vijana watatu waliokamatwa, walitoka Kigoma kuja Kibaha kufanya kazi ya ulinzi kwenye mashamba, huyu mkazi wa kibaha kijiji cha kidimu anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumteka msichana wa hapo kijijini kwa miezi minne kabla ya ishu kufumuka february 26 baada ya binti kupata upenyo na kutoroka.
Kwenye
hayo matofali hapo ndipo alipokua analazwa binti alietekwa na kutumika
kingono, mwanaume alikua akimaliza haja yake ndio anamrudisha humo
ndani, vijana waliohusika ni watatu na wanashikiliwa na polisi
tayari kwa kufikishwa mahakamani, stori itaendelea leo kwenye Leo Tena
ya Clouds Fm.
Huyu
ndio binti mwenyewe wa miaka 16 alietekwa, alipata ujauzito wa miezi
miwili lakini vijana hao wakautoa kwa kutumia majani ya chai
Akionyesha sehemu aliyokua analazwa.
Huyu
binti alipotea toka novemba 2012 na alishatafutwa kila sehemu ikiwa ni
pamoja na waganga kutumika, wazazi walishaomba sana kanisani na kukata
tamaa wakijua binti yao ameshakufa mpaka wakaweka msiba kabisa.
Picha na taarifa vimetoka kwa dinamarios.blogspot.com
No comments:
Post a Comment