http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Friday, March 1, 2013

Wanariadha watatu wapigwa marufuku Kenya

Baada ya kuenea uvumi kuhusu ripoti za wanariadha kutumia dawa za kusisimua misuli, wanariadha watatu wakenya wamepigwa marufuku baada ya kugunduliwa kutumia dawa hizo.

Wanariadha wa mbio za marathon Wilson Erupe Loyange na Nixon Kiplagat Cherutich watatumikia adhabu ya kutoshirikia katika mashindano yoyote kwa miaka miwili. Moses Kiptoo Kurgat amepigwa marufuku wka mwaka mmoja.
Mwanariadha wa nne Francis Kibiwott, ambaye alimaliza katika nafasi ya 45 katika ubingwa wa mbio za nusu marathon za mwaka wa 2007 nchini Italia aliondolewa shutuma baada ya kesi yake kutathminiwa na tume ya matibabu ya shirikisho la riadha duniani IAAF.
Kenya inayofahamika kutamba katika mbio za masafa ya kadri na marefu, imekuwa ikishutumiwa kufuatia ripoti za kuwepo matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku miongoni mwa mwanariadha wake maarufu. Katibu mkuu wa shirikisho la riadha Kenya David Okeyo amesema hawatawasamehe wanariadha watakaogundulika kutumia dawa hizo.

No comments:

Post a Comment