http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Friday, March 1, 2013

msome Ryan Giggs aliko tokea

KWENYE kumbukumbu ya maisha ya Ryan Giggs kuna mstari umeandikwa hivi: “Meneja alikuwa mtu mmoja anaitwa Dennis Schofield, mtu wa soka kweli… Dennis alikuwa muuza maziwa, lakini vipi alizunguka hilo hakuna anayelijua. Alikuwa hawezi kupita mahali akakuta watu wanacheza soka halafu aache kuangalia.”
Kwenye index ya kitabu hicho, jina la Schofield liko kati kati ya jina la Peter Schmeichel na Paul Scholes. 
Wakati mchango wa Schofield kwa Giggs na Manchester United ya kisasa hautendewi haki. Siku zote kuna mtu anayeona kwa mara ya kwanza, na mtu wa kwanza kuona kipaji cha asili cha Giggs alikuwa ni muuza maziwa Swinton ambaye anatajwa kama msaka vipaji wa Manchester City. 

Diamond: Dennis Schofield (right) found Ryan Giggs (left) and still coaches kids in Salford today
Almasi: Dennis Schofield (kulia) alimvumbua Ryan Giggs (kushoto) ni kocha wa vijana wa Salford 

TAKWIMU ZA RYAN GIGGS

Kuzaliwa: Nov 29, 1973, Cardiff 
Mataji
Man Utd:
 Ligi Kuu ya England (12): 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11 
Kombe la FA (4): 1993–94, 1995–96, 1998–99, 2003–04 
Kombe la Ligi (4): 1991–92, 2005–06, 2008–09, 2009–10
Ngao ya Jamii (8): 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010 
Ligi ya Mabingwa Ulaya (2): 1998–99, 2007–08 
Super Cup (1): 1991 
Intercontinental Cup (1): 1999 
Kombe la Dunia la Klabu (1): 2008
Tuzo nyingine
OBE for services to football: 2007 
BBC Sports Personality of the Year: 2009
CRAIG WALL
Akiwa na miaka 82, Schofield bado yuko fiti na ni rais wa Klabu ya Vijana ya Deans, timu ambayo ilimshawishi Giggs kujiunga nayo miaka 30 iliyopita.
Giggs hajawahi kusahau hili; ni mlezi wa klabu hiyo na amefungua uwanja wao mpya siku za karibuni. Pamoja na Schofield kumfurahia Giggs, kucheza mechi 1,000, hatahivyo mzee huyo bado anajuta kwanini winga huyo wa kushoto hakujiunga na timu yake Man City.
Sasa hivi historia ya soka la Jiji la Manchester Ingekuwa tofauti sana.
Schofield anaamini Giggs anaweza kucheza kwa muda mrefu kama Stanley Matthews, lakini yeye kumbukumbu yake ipo kwa kijana mdogo aliywemvumbua.
“Nilikuwa muuza maziwa wakati huo, na nilikuwa mfanyakazi wa Man City pia,”  Schofield alikumbuka jinsi alivyomuona Giggs kwa mara ya kwanza.
“Siku moja niliona vijana wakitoka shule wakiwa na viatu vyao. Walikuwa na umri wa kama miaka nane na tisa, nikawauliza kama walikuwa wanaenda kucheza mechi.
“Nikaongozana nao kwenda kuwaangalia na nikamuona kijana mmoja kwenye winga ya kushoto alikuwa kama Swala, baruti. Alikuwa ni Ryan Wilson, kwa wakati huo, muda siyo mrefu akahamia Swinton akitoka Wales. 
“Nikamuuliza mmoja wa walimu wake, kama wazazi wake walikuwa uwanjani. Wakasema mama yake alikuwepo. Nikamfuata na kumuuliza: ‘Yule ni mwanao kwenye winga ya kushoto?’ Akajibu ndio nikamuuliza kama angependa kuja kwenye klabu yetu, Deans. 
“Nilikuwa nafikiria mwenyewe: ‘Simkosi huyu.’”

Stars of the future: Giggs with coach Eric Harrison (left) Nicky Butt, David Beckham, Gary Neville, Phil Neville, Paul Scholes and Terry Cooke in 1995
Mastaa wa baadaye: Giggs akiwa na kocha Eric Harrison (kushoto) Nicky Butt, David Beckham, Gary Neville, Phil Neville, Paul Scholes na Terry Cooke mwaka 1995
And now: Giggs (left) scored against Queens Park Rangers last weekend
Na sasa: Giggs (kushoto) alifunga dhidi ya Queens Park Rangers mwisho wa wiki iliyopita

NAMBA ZA GIGGS 

168  Mabao ya Giggs kwenye mechi 931akiwa na Man United
149 Wachezaji aliowahi kucheza nao United, 
16  Mchezaji pekee kufunga kwenye michuano 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 
127 Giggs ni mchezaji aliyetoa pasi nyingi zaidi za mabao kwenye Ligi Kuu ya England akiwa amefanya hivyo mara 127.  
“Alikubali na nikamwambia nitamchukua Ryan (Giggs) Alhamisi kwa ajili ya kwenda mazoezini. Alijiunga nasi na kila mtu aliweza kuona jinsi gani alikuwa na kipaji, alikuwa na tabia nzuri na kila mtu alimpenda.
“Aliomba kaka yake Rhodri ajiunge nasi na kweli alijiunga na sisi. Kila mtu alimpenda.
“Ryan (Giggs) alijiunga na timu yetu ya vijana wa miaka tisa na alikuwa bora. Umiliki wake wa mpira kasi – kumbuka bao alilolifunga dhidi ya Tottenham miaka yote hiyo iliyopita alikuwa na vitu hivyo.” Alisema Schofield
Schofield aliwahi kufanya majaribio na Bolton na kuna wakati aliwahi kucheza na John Charles kwenye Kombe la British Army. 
Alipoanza kazi ya kusaka vipaji anasema alikuwa akiweza kuona kipaji ambacho mtu mwingine asingeweza kukiona. Naweza kumjua mcheza na mtu asiye mchezaji, na Ryan siku zote alikuwa mchezaji.”

Been there, done that: Giggs (right) holds the Champions League trophy in 2008 after beating Chelsea
Mafanikio: Giggs (kulia) akiwa amebeba taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2008 baada ya kuichapa Chelsea, jijini Moscow
Iconic: Giggs scored the winning goal in the 1999 FA Cup semi-final to see off Arsenal
Gwiji: Giggs alifunga bao la ushindi mwaka 1999 wakati wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal 
Kutoka timu ya vijana ya Deans, Schofield alimpeleka Ryan Wilson kwenye klabu ya Manchester City. Alikuwa na matumaini kwamba Man City watamsajili kinda huyo, japokuwa kwenye kitabu chake Giggs anasema alikuwa akitamani kuchezea Man United.
“Kwa miaka kadhaa tulikuwa tukenda Isle of Wight kwa ajili ya micuano ya mwisho wa wiki.” Alisema Schofield
“Mara ya kwanza kumpeleka Giggs kila mtu alihoji: ‘Nani huyu” mwaka uliofuta tulimpeleka tena watu waliacha kuangalia mechi waliyokuwa wakitazama kuja kuimsangaa Ryan. 
“Huo ni ukweli, Scholes na ndugu wawili wa Neville walikuwemo kwenye michuano hiyo na timu yao ya Oldham, lakini hakuna aliyeng’ara zaidi ya Ryan. Alikuwa kwenye sayari yake.
“Akiwa na miaka tisa nilimpeleka Man City. Walimtayarishia zuria jekundu, wale wachekeshaji Little na Large, ambao ni mashabiki wakubwa wa City, nao pia walimtandikia zuria jekundu. Kwa miaka mingi kulikuwa na picha kwenye ukuta wa Man City ikimuonyesha Ryan akichezea timu yao.
“Walikuwa wakisema kwamba atakapo saini mkataba akiwa na miaka 14 watakuwa wamelamba dume.”


Winner: Giggs lifts the Premier League trophy in 2008 after helping United to years of dominance
Ubingwa: Giggs akinyanyua taji la Ligi Kuu ya England mwaka 2008
Stalwarts: Giggs and Rio Ferdinand (right) parade their spoils on the pitch at Old Trafford
Mashujaa: Giggs na Rio Ferdinand (Kulia) wakiwa na mataji ya ubingwa kwenye uwanja wa Old Trafford 
Fresh faced: A young Giggs poses alongside Eric Cantona in 1994
Kinda: kijana Giggs akiwa kwenye picha na Eric Cantona mwaka 1994
“Nilimwambia Ken Barnes (Mkuu wa wasaka vipaji wa Man City) kwa wakati huo: “Siku Ryan akitimiza miaka 14 hakikisha uko nyumbani kwao kwa sababu Man United wanammendea.”
“Akajibu kwamba Man City wameshaongea na wazazi wa Ryan na kila kitu kiko poa. Asubuhi ya siku ya kuzaliwa ya Ryan akitimiza miaka 14, Alex Ferguson na msaka vipaji wake Joe Brown walifika nyumbani kwao na kwa ajili ya kumsainisha.
“Watu wa Man City walikuwa ofisini kwao. Kwa aina ya mchezaji kama yeye unatakiwa kuwa wa kwanza, kufika nyumbani kwao na kuwawahi wapinzani wako. Ryan alikuwa shabiki wa Man United, lakini nilisikitishwa sana na Man City, nikaachana nao kutokana na hilo.”
Kupitia kwa Blackburn Rovers, pamoja na Brian Kidd, na msimu mmoja Man United, Schofield amerudi Man City, ni mtu wa Mjini anayejua kufanya kazi kwenye Jiji la Manchester na kuna ukweli pale aliposema: “Ferguson aliwazidi kete tena kwa kijana wa miaka 12, 13 ambaye ni mchezaji mzuri pia.

Proud: Schofield is glad to see Giggs grow into the superstar he has become today
Anajivunia: Schofield anajivunia kumuona Giggs supastaa leo
“Nilimpendekeza kwa Man City, lakini United walikuwa wa kwanza kufika – unatakiwa kufika wa kwanza, japokuwa wazazi wake ni watu wa Man United.”
Hata katika umri wake huu Schofield anatabia kama za Ferguson na kijana aliacha shughuli zake za kuuza maziwa na kwenda kumcheki miaka 30 iliyopita sasa ni staa.
“Nimekuwa nawasilina na Ryan siku zote, bado huwa anakuja klabuni kwetu akiwa na muda, nimemuona akikua na kuwa Supastaa.” Alisema Schofield.

No comments:

Post a Comment