Wakazi wa jiji la mwanza wapagawishwa na avamizi FEKI wa Ali-Shabaab uliofanyika ndani ya Hotel ya Gold Crest
Wakazi wa jiji la Mwanza juzi majira ya saa 4 asubuhi waliwekwa njia
panda na kujawa hofu kubwa kufuatia vikosi vya askari kanzu, FFU, askari
polisi na zimamoto wakiwa na vifaa sambamba na magari yao walipolivamia
jengo la Hotel Gold Crest na kuanza saka saka za kujiweka sawa huku
wakiendeleza mapambano na jamaa ambao walijipanga mithili ya wahalifu.Hali hiyo ilisababisha magari pikipiki kusimama kwa muda huku
wananchi wakiingiwa hofu na woga, wengine wakikimbia na baadhi ya
Hata
hivyo mpaka zoezi hilo linamalizika hakuna mwananchi aliyeweza kubaini
kuwa tukio hilo lilikuwa ni la uigizaji, kila mmoja alikuwa
akisimulia kivyake sekeseke zima, lakini mapango mzima ulikuwa ni
kuvinoa vikosi vya polisi na Zimamoto juu ya kukabiliana na uhalifu
kwenye majengo makubwa ya huduma mbalimbali.
Wateja wa kituo cha mafuta kilichopo karibu na hotel Gold Crest jengo
ambalo ndiko zoezi lilikuwa likifanyika pamoja na wateja wa ofisi za
PPF, duka la Vodacom Mwanza na Benki ya NMB zilizopo katika jengo hilo
walikosa huduma kwa muda huku wengine wakitimka maeneo hayo kwa
tahadhari wakidhani ni live.
Watu wakihaha nao polisi wakiweka ulinzi mkali eneo la tukio.
Harakati zikiendelea eneo la tukio.
Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi 'wahalifu bandia' katika zoezi lililozua taharuki kwa kwakazi wa jiji laMwanza.