MSHAMBULIAJI
Robin van Persie amekuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi
kufutaia kufunga mabao matatu peke yake (hat trick) usiku huu katika
ushindi wa 8-1 dhidi ya Hungary.
Mshambuliaji
huyo wa Manchester United aliingia katika mchezo huo wa kufuzu Kombe la
Dunia mwakani nchini Brazil, akiwa ana mabao 38 katika mechi 78 za
Orange, na wenyeji hawakuwa na presha kwa kuwa walikwishajihakikishia
tiketi ya Brazil Septemba mwakani.
Van Persie alifunga dakika ya 16 kabla ya Kevin Strootman na Jeremain Lens kuongeza.
Nahodha
wa The Orange akafikia rekodi ya mabao 40 ya Patrick Kluivert karibu na
mapumziko na akashangilia kwa kumkumbatia Kluivert, ambaye ni mmoja wa
wasaidizi wa Louis van Gaal katika timu hiyo.
Van
Persie akavunja rekodi hiyo kwa bao la dakika ya 53 baada ya kazi nzuri
ya Arjen Robben -- ambaye pia alimpa van Persie pasi ya bao la pili
kabla ya kumpisha Dirk Kuyt dakika ya 61, Uholanzi wakiibuka na ushindi
mnono wa mabao 8-1.
Mabao
mengine ya Uholanzi yamefungwa na Strootman dakika ya 25, Jens dakika
ya 38, Devecseri akajifunga dakika ya 65, Van der Vaart dakika ya 86 na
Robben dakika ya 90, wakati la Hungary lilifungwa na Dzsudzsak kwa
penalti dakika ya 47.
Kiwango cha dunia: Robin van Persie sasa ni mfungaji bora wa kihistoria Uholanzi
Kitaalamu: Van Persie ni miongoni mwa wamaliziaji bora duniani
Daka kama unaweza: Van Persie akifunga kwa ustadi wa hali ya juu
Hata kwa vichwa: Van Persie akifunga kwa kichwa
Wakati wa kushangilia: Wachezaji wa Uholanzi wakishangilia ushindi wao wa 8-1
Hata huyu mbaya: Jeremain Lens akiifungia Uholanzi bao la tatu
Wachezaji wa Uholanzi wakipongezana
Ameondolewa kileleni: Patrick Kluivert ndiye alikuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi
Katika mchezo mwingine, bao pekee la
Andriy Yarmolenko dakika ya 64 limeipa Ukraine ushindi wa 1-0 dhidi ya
Poland na kufufua matumaini ya kucheza Kombe la Dunia.
Mshindi wa mechi: Andriy Yarmolenko akishangilia bao pekee dhidi ya Poland
Nayo Ubelgiji imejikatia tiketi ya
kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002
baada ya mshambuliaji anayecheza kwa mkopo Everton kutoka Chelsea,
Romelu Lukaku kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya
Croatia.
Matokeo hayo yanamaanisha vinara hao wa
Kundi A, Ubelgiji hawawezi kukamatwa kwa pointi zao 25 walizovuna kwenye
mechi tisa wakiwa wamebakiza mechi moja nyumbani na Wales Jumanne.
Shujaa: Mabao mawili ya Romelu Lukaku yameipeleka Ubelgiji Fainali za Kombe la Dunia mwakani
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Alberto
Aquilani alifunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi Italia ikitoa
sare ya 2-2 na Denmark katika mchezo wa Kundi B.
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas
Bendtner alifunga mabao mawili na kuwafanya waongoze 2-1, lakini ambayo
tayari imekwishafuzu ilipata mabao yake kupitia kwa Daniel Osvaldo na Aquilanina kuiongezea ugumu Denmark wa kwenda Brazil.
Kitu hicho: Nicklas Bendtner akimtungua kipa wa Italia, Gianluigi Buffon na kufanya 1-1
Shangwe: Bendtner akishangilia bao lake la kwanza na beki wa Liverpool, Daniel Agger
No comments:
Post a Comment