walio vifua wazi ni wachezaji wa timu ya taifa Tanzania
Pichani ni aliyekuwa Rais wa Sudan, Bwana Jaafar Mohammed Numeir (Wa kwanza Kulia Mwenye Suti) akiongozwa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Bwana Abdulrahman Juma (Katikati Mwenye Kaptula Nyeupe) kusalimiana na Mchezaji wa Nguli wa Taifa Starz Bwana Omar Zimbwe huku Wachezaji wa Taifa Starz wakiwa Vifua wazi bila Jezi.
Wa Kwanza Kushoto anayeangalia ni Mchezaji Mohamed chuma "Shoto" na wanaonekana nyuma ya Nahodha Abdulrahman ni Wachezaji Mashuhuri Kitwana Manara "Popat" na Abdallah "King" Kibaden Mputa, hapa ilikuwa katika Uwanja wa Uhuru (Uwanja wa Zamani wa Taifa, Jijini Dar es salaam).
Watu wengi wanapenda kuandika kuwa Mechi hii Taifa Stars walicheza vifua wazi (Bila Jezi) na sudan baada ya kukosekana jezi, Lakini ukweli wa mambo haukuwa hivyo bali kilichotokea ni kuwa Timu zote Mbili zilikuja Uwanjani zikiwa na Jezi zinazofanana.
Kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Shirikisho la Soka Duniani, FIFA ni kwamba kunapotokea Timu mbili zina jezi zinazofanana basi ile ambayo iko nyumbani (Wenyeji) ndiyo inatakiwa ibadilishe jezi, Taifa Stars hawakwenda Uwanjani na Jezi za Ziada.
Mara baada ya Ukaguzi uliofanywa na Rais Jaafar Mohammed Al- Numeir wa Sudan Starz waliletewa Jezi Nyengine na ndipo Mpira ukaanza huku Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa Uwanjani hapo kushuhudia Aibu hiyo ya Mwaka.

No comments:
Post a Comment