Baada ya kuvishwana pete ya uchumba, wasichana wengi huona kwamba
kilichoko mbele yao ni kupanga harusi tu. Hujishughulisha kwa hali na
mali kuhakikisha harusi inakuwa sawa na ile anayoiwaza siku zote, na
kusahau kuwa baada ya harusi kuna maisha ambayo ndiyo haswa yanayopaswa
kupangiliwa kwa umakini. Baadaye wanajikuta wameingia kwenye ndoa huku
mambo mengi yakiwa hewani na hivyo kupelekea migogoro isiyoyalazima mara
tu baada ya ndoa.
Kuna mambo muhimu sana ambayo wachumba
wanapaswa wayaongelee na kufikia muafaka kabla ya kuunganika na kuwa
mwili mmoja. Yanaonekana ya kawaida sana lakini yanaweza kuleta msuguano
na kuharibu kabisa furaha ya ndoa. Tuyaangalie kwa uchache:
1. Mahali pa kuabudu.
Binti anaabudu katika kanisa kubwa na ndiye kiongozi wa sifa na
muongozaji wa nyimbo karibia zote za kwaya, na kijana anaabudu kwenye
kanisa dogo linaloanza na ndiye mwenyekiti wa vijana na mwalimu wa shule
ya jumapili. Hapa nani anamfuata nani? Bila kukaa chini na kujadiliana
kwa pamoja jambo hili linaweza kuleta mvutano. Ni vyema mkaangalia kwa
mapana na marefu option zote kisha kwa pamoja mfikia muafaka kulingana
na huduma ya kila mmoja wenu.
2. Jinsi ya Kuishi Waafrika
ni kawaida yetu kuishi pamoja na ndugu zetu na kusaidiana katika mambo
mbalimbali ya maisha. Sio jambo geni kumkuta kijana au msichana anaishi
na wadogo zake na kuwasomesha. Linapokuja suala la ndoa ni vyema jambo
hili likawekwa sawa mapema. Je mtaweza kuishi na ndugu wangapi? Na wa
upande upi na kwa kigezo gani? Je wataanza kuishi nanyi muda gani baada
ya kuoana? Pale tu mtakapooana au lini? Hili si jambo dogo na linaweza
kuharibu amani kabisa ndani ya nyumba. Ni vyema mkaliweka sawa mapema na
wale mnaoishi nao wajue hawaishi tena na kaka au dada bali Mr & Mrs
hivyo heshima iwe kwa wote. Pia sishauri kuishi nao mara tu baadavya
kuoana, ni bora wakaenda kwa ndugu wengine angalau mwezi mmoja wa kwanza
muweze kuwa na wakati wenu wa faragha wa kufahamiana vizuri na kuizoea
nyumba yenu mkiwa wenyewe.
3. Mapato na Matumizi Hili ni
eneo nyeti sana. Wasichana wengine wanapoolewa huambiwa kuwa ‘usimwambie
mumeo unapata kiasi gani na uwe na akaunti yako ya siri.’ Mmh hapa pana
tatizo, maana nijuavyo mimi mwili mmoja ni katika kila idara, hamna
siri. Sasa wewe ukificha na mwenzio akaficha, kuna maendeleo kweli hapo?
Ni muhimu sana kwa wachumba kukaa na kupanga jinsi ya kuyatumia mapato
yenu mtakapooana. Muwe wawazi kila mmoja anachokipata na muainishe
matumizi yenu na kuangalia ni kwa jinsi gani mtaweza kuyafanikisha.
Baada ya kuoana, kila kitu kitakuwa ni chenu wote. Kama ulikuwa na
nyumba, gari, viwanja, shares, bank accounts n.k vyote vinakuwa mali ya
familia, hivyo ni vyema mkaangalia hili mapema ili asije mmoja wenu
akajenga nyumba kwa siri bila mwenzie kujua. Pia muangalie ni ndugu gani
wanahitaji msaada kifedha na jinsi gani mtaendelea kuwasaidia, mfano
ada, matibabu, n.k. Hapa panahitaji hekima kubwa sanabya kiMungu kuamua
nani asaidiwe kulingana na kipato chenu kwa wakati huo. Maana ndugu wa
kuhitaji msaada wenu watakuwa ni wengi kuliko uwezo wenu. Hapa ndipo
mstari wa mithali 14:1 unapoleta maana. Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
4. Mipango ya Mbeleni
Shule, ujenzi, kuanzisha familia, kufungua biashara, kuanzisha huduma
n.k yote haya yanahitaji kuzungumziwa mapema na kuwekewa misingi. Mfano
wewe unahitaji baada tu ya ndoa utafute scholarship ukasome ulaya wakati
mwenzio akifunga macho tu anajiona anaitwa baba, hapo lazima shida
itatokea. Lazima mjue vipaumbele vyenu kama familia ni nini.
Mkishafahamu hilo ni rahisi kujua muanzie wapi na wakati gani. Mume
hawezi tu kuamka asubuhi na kusema anaacha kazi na kuanzisha kanisa,
sasa familia itakula wapi? Ni lazima mkae chini mpange mjue mume akiacha
kazi familia itaishije, mke je atakuwa tayari kubeba majukumu yote?
Mwisho huu ndio wakati muafaka kumweleza mwenzio kama uliwahi
kuchumbiwa hadi kutolewa mahari lakini mambo yakaharibika. Pia kama
unamtoto ni lazima narudia LAZIMA umweleze mwenzi wako. Usiingie kwenye
ndoa na siri yoyote, itakuwa ni bomu la kuwasambaratisha.
No comments:
Post a Comment