http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Friday, March 1, 2013

UHURU SELEMANI ATEMWA KWENYE KIKOSI KIENDACHO SUDAN KWA AJILI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Azam FC wanatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho mjini Dar es Salaam kwenda Sudan Kusini, tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho dhidi ya wenyeji, Al Nasir Juba.
Kocha Msaidizi wa Azam, Kalimangonga Sam Daniel Ongala ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, timu iko vizuri na wana matumaini makubwa ya kwenda kushinda na ugenini pia.
Kali alisema kwamba wanawaheshimu wapinzani wao na hawatawadharau hata kidogo, bali watakwenda kucheza kwa juhudi kuliko walivyocheza kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita, ambayo walishinda 3-1 nyumbani Dar es Salaam.


“Tunakwenda kucheza kwa ajili ya kushinda, hatuendi kufanya mzaha, haya ni mashindano na kila timu inayoingia hapa maana yake ni nzuri,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
Aidha, Kali alitaja kikosi cha wachezaji 20 kinachoondoka kesho kuwa ni makipa; Mwadini Ally na Aishi Manula, mabeki; Joackins Atudo (Kenya), David Mwantika, Himid Mao, Malika Ndeule, Waziri Salum na Luckson Kakolaki.
Kwa upende wa viungo ni Kipre Balou (Ivory Coast), Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar, Humphrey Mieno (Kenya), Abdi Kassim ‘Babbi’ na Khamis Mcha ‘Vialli’ wakati washambuliaji ni John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche (Ivory Coast), Seif Abdallah, Brian Umony (Uganda) na Gaudence Mwaikimba. 
Aliwataja wachezaji watano walioachwa kuwa ni kipa Jackson Wandwi, mabeki Omar Mtaki na Samih Hajji Nuhu na viungo Abdulhalim Humud na Uhuru Suleiman.
Azam inahitaji sare yoyote katika mchezo huo wa Jumapili ili kusonga mbele, baada ya ushindi wa 3-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza na hata ikitokea bahati mbaya ya kufungwa, basi isiwe kwa tofauti ya zaidi ya bao moja.

No comments:

Post a Comment