Mheshimiwa  Balozi Hamisi 
Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka 
Lichinga  nchini Msumbiji waliofika katika maadhimisho hayo.
 
………………………………………………………………….
Maadhimisho ya Tamasha la 
Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni Kitaifa yamekuwa 
yakiadhimishwa kila mwaka tarehe 27 Februari, Mkoani Ruvuma kuanzia 
mwaka 2010.  Dhana ya maadhimisho haya ni kufanya  Kumbukizi za Vita ya 
Majimaji ziwe kichocheo cha mabadiliko kwa jamii kifikra na 
Kiutamaduni.  Kuwaleta pamoja wadau wa historia ya Vita vya Majimaji
Pia kuwakumbuka Mashujaa  wa 
Vita vya Maji Maji walionyongwa tarehe 27 Februari,1906 na Wajerumani 
ambao wamezikwa katika eneo la Makumbusho ya Kumbukizi ya Vita vya 
Majimaji – Songea
Vilevile Kutoa fursa kwa jamii 
kushiriki katika kuenzi na kuendeleza urithi wetu  kupitia shughuli za 
kimila zinazofanywa na Wazee  wa Baraza la Mila na desturi za jamii 
iliyohusika katika tukio la Vita vya Maji Maji.
Na kutoa elimu kwa Umma wa Watanzania kwa ujumla kuhusu Kumbukumbu za Kimakumbusho kupitia matukio ya kimila na kihistoria.
Kuweka dhahiri madhumuni ya kuanzishwa kwa Makumbusho ya Taifa nchini kwa vitendo.
Katika maadhimisho haya Waziri 
wa Mali asili na utalii Dkt.Hamis Kagasheki ameitaka jamii nchini kuenzi
 harakati hizo zilizofanywa na mababu wa taifa hili katika kupinga 
utawala wakikoloni.
Pia amesema amefurahishwa kuona 
kuwa maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya majimaji yamekuwa na historia 
ya kuadhimishwa mwezi februari Mkoani Ruvuma katika ngazi ya mkoa tangu 
nchi yetu ipate uhuru, Hii imelenga kuwakumbuka  Mashijaa wa Vita vya 
Maji Maji.
Hii imeonyesha kwa jinsi Uongozi
 wa mkoa , Wazee wa Baraza la Mila na Desturi na wananchi wanavyothamini
 mchango waliokuwa nao Mashujaa hawa hata kujitoa mhanga kutetea uhuru, 
haki na utawala wao pamoja na kulinda mila , tamaduni na rasilimali 
zilizopatikana kwenye maeneo yao kwa manufaa ya jamii na taifa kwa 
ujumla.
Hili ni jambo la kuigwa na kila mtu kuthamini na kulinda urithi wetu wa utamaduni kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijazo.
 Akiendelea kusema ameshuhudia 
kuwepo kwa taarifa za mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama 
Mkomanile ambaye alishiriki katika harakati hizo za mapambano dhidi ya 
utawala wa kikoloni hivyo ni ishara kuwa akina mama nao walishiriki 
kikamilifu katika mapambano hayo dhidi ya ukoloni ambapo kwa upande wa 
Tanganyika ilikuwa ni Vita ya Maji maji ,na kwa upande wa Kenya ilikuwa 
ni Mau mau na vyote vilikuwa ni chanzo cha vuguvugu la ukombozi wa bara 
la Afrika.
Pia ametoa wito kwa wadau wa 
utafiti kufanya utafiti zaidi  habari za mwanamke huyo ili nazo ziweze 
kuingizwa kwenye historia ya kumbukizi hiyo ya vita ya Maji Maji ambayo 
pia ilikuwa ni chachu ya ukombozi wa bara la Afrika kwa ujumla.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi.
 Baadhi ya wazee  wakiwa wameshika 
Silaha za Jadi walizotumia mababu zetu kupigania dhidi ya kupinga 
utawala wa Wakoloni wa Kijerumani
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Kamanda wa Jeshi la wananchi akiweka upinde
Mpiganaji wa vita kuu ya pili ya Dunia 
Mzee Komba akisindikizwa na kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania 
kwenda kuweka shahada ya uwa katika mnala wa mashujaa.
 Hii ni kwa nje ndivyo hali ilivyokuwa
 Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri 
wa Maliasili na Utalii pamoja na viongozi wengine wakitoa salamu ya 
heshima kwa mashujaa wa majimaji
Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezi kwa njia ya kijeshi
 

 
No comments:
Post a Comment