Mshambuliaji huyo wa Liverpool alinaswa
na kamera za Televsheni akimrupia konde mchezaji wa Chile, Gonzalo Jara,
lakini Nestor Pitana, Ofisa wa mechi hakulinukuu tukio hilo, baada ya
kuzungumza na wawili hao kufuatia kuvurugana kwao wakati wa kona.
Ikiwa itabainika ni kweli alifanya
hivyo, Suarez atakuwana na rungu la FIFA ingawa haiwezi kufanya hivyo
hadi ipate ripoti rasmi ya refa ya maandishi.

Tukio: Luis Suarez akimchapa konde Gonzalo Jara usoni.

Kifungoni: Suarez tayari atatumikia adhabu ya kadi za njano.
Msemaji wa FIFA amesema: "Tutaendelea
kukusanya ripoti zote za mechi, kwa kuwa marefa wana saa 24 ya
kuwasilisha ripoti hizo. Tutaangalia kilichomo kwenye ripoti zao, kisha
FIFA itachukua hatua kwa mujibu wa ripoti hizo."
Suarez tayari anakabiliwa na adhabu ya
kusimamishwa baada ya kupewa kadi ya njano dakika za lala salama katika
medhi dhidi ya Chile kwa utovu wa nidhamu.
Atakosa mechi ijayo ya Urugay dhidi ya
Venezuela mwezi Juni kuwania Fainali za Brazil, ambayo ni habari njema
kwa klabu yake Liverpool.
No comments:
Post a Comment