Kidawa Wa Enzi
Ulichonacho azizi Tamka usikilike
Yangu yote machozi Yatoke na yatumike
Na iwe kwangu ajizi Sijali wache wacheke
Mpenzi wangu wa Enzi Kidawa afahamike.
Kidawa wangu mlinzi Wa moyo akubalike
Wako mie mwanafunzi Tayari nisomesheke
Kufa mie kwa kitanzi Kidawa sibadilike
Mpenzi wangu wa Enzi Kidawa afahamike.
Kula mekosa utamu Wacheni nibabaike
Kusahau ya muhimu Mja nidhadhalilike
Kazi kwenu kufahamu Kidawa ahadithike
Mpenzi wangu wa Enzi Kidawa afahamike.
Ahadithike Kidawa Mauti yasimfike
Mwaka wakupagawa Kiumbe niadhirike
Singetibika kwa dawa Waganga wafaidike
Mpenzi wangu wa Enzi Kidawa afahamike.
Jueni Penzi hatiya Kidawa msimshike
Najisikia vibaya Yangu msiyaanike
Si shilingi si rupiya Penzi halina makeke
Mpenzi wangu wa Enzi Kidawa afahamike.
Sitaki masuali,kwa kuwa sina majibu ,hahahaaa!
No comments:
Post a Comment