JKT
Ruvu ya Pwani, imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Toto Africans
ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
Ushindi
huo, unaifanya JKT Ruvu itimize pointi 19, baada ya kucheza mechi 18,
na kujiondoa kwenye maeneo ya hatari ya kushuka daraja.
Kwa
upande wa Toto, ambayo sasa inabaki na pointi zake 14 licha ya kucheza
mechi ya 19 leo, kipigo hicho kinazidi kuwachimbia kaburi kwenye msimamo
wa Ligi Kuu.
Katika
mchezo huo, uliokuwa wa vuta nikuvute, Wana Kishamapanda ndio waliokuwa
wa kwanza kupata bao dakika ya 26, mfungaji Mwinja Magafu, ambalo
lilidumu hadi mapumziko.
Maafande
wa Jeshi la Kujenga Taifa, walisawazisha bao hilo dakika ya 52 kupitia
kwa Ally Khan, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan
Mgosi kuifungia bao la ushindi timu yake dakika ya 71.
No comments:
Post a Comment