http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Tuesday, July 23, 2013

Rais Kikwete aongoza waombolezaji kuaga miili saba ya wanajeshi waliouawa Darfur.


 Amirjeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Kikwete akiongozana na viongozi mbalimbali waandamizi katika serikali ya jamhuri ya muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na watu maarufu amewaongoza mamia ya waombolezaji katika kuiaga miili saba ya wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania waliouwawa nchini Sudan Jumamosi ya July 13 mwaka huu.
Dr Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo akionekana dhahiri shairi mwenye majonzi  ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kuwaongoza mamia ya waombolezaji kuiaga miili ya wanajeshi hao waliouwawa na kikundi cha waasi nchini Sudan katika jimbo la Darfur amesema taarifa za tukio hilo limemuhuzunisha,kumsikitisha na kumkasirisha na kushauri kuwa wakati umefika wa kuutazama upya mfumo mzima wa kulinda amani Darfur hasa kuhusu kiwango cha uwezo wa wanajeshi kujilinda kutokana na ukweli kuwa tayari walinda amani 41 kutoka mataifa mbalimbali wameuwawa na wengine 55 kujeruhiwa.
Aidha waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Mh Shamsi Vuai Nahodha amekiita kitendo cha wanajeshi hao wakulinda amani kuuwawa ni dhahiri tendo ovu ambao ni mkakati maalum wa waasi kutaka kuhakikisha mpango wa umoja wa mataifa katika kuleta amani katika nchi zenye mifarakano hazifanikiwi huku salamu za rais wa mapinduzi ya Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein zikisomwa na mwakilishi.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi hapa nchini jenerali Davis Mwamunyange amesema wanajeshi hao walishambuliwa na waasi wakati wakisindikiza na kutoa ulinzi kwa waangalizi wa amani na washauri wa polisi na kwamba walipopunguza mwendo kutokana na utelezi uliosababishwa na mvua umbali wa kilomita 25 kutoka Darfur ndipo waliposhambuliwa.
Zoezi hilo la kuiaga miili ya mashujaa hao waliouwawa nchini Sudan mbali na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali waandamizi serikalini pia limehudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dr Regnald Mengi huku aliyekuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr Asha Rose Migiro akisema tukio hilo lisiwakatishe tamaa katika kupigania amani ya watu wengine katika nchi zenye mifarakano.

Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Majeneza yenye miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Bilal, na viongozi wengine wakiwa katika shughuli hiyo ya kuagwa miili ya askari hao leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga Dar es Salaam. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. Kulia ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Majeneza yenye miili yakiwa eneo la tukio tayari kuagwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Mkuu wa Majeshi,Jenerali Davis Mwamunyange, akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya Askari pia wakiwa na nyuso za huzuni.

No comments:

Post a Comment