Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe akiwa kizimbani. Yusufu akificha sura yake asipigwe picha baada ya hukumu ya miaka 30.Kulia
ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake
wakati wakitoka mahakamani. Kushoto ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na
kuzalishwa.
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu
kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani
kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka
15( jina linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka wa serikali Archiles
Mulisa aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa
Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa
kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria
kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai
kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada
ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo
alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la
Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa miaka minne hadi ilipogundulika
kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni
kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya
kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani
kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia
hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni
binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa
Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali
baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa
ulidai kuwa Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15
ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa
asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu, Hakimu alimpa
nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa
kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la
kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu
Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata
rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo,
Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na
Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume
mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “mfa
maji haachi kutapatapa”
HABARI NA MBEYA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment