http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Sunday, June 16, 2013

MABOMU&KIOJA KILICHOTOKEA UWANJA WA TAIFA HII LEO

Tanzania Vs Ivory Coast

Kila la heri Taifa Stars
timu ya taifa ya tanzania hii eo imeshindwwa kuonesha cheche zake  katika uwanja wake wa nyumbani kwa kukubali kipigo cha mabao manne kwa kwa mawili, japokuwa taifa stars ilionesha kumiliki mpira kwa muda mrefu uku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Thomas Ulimwengu.
UDHAIFU
udhaifu umekuja kujitokeza katika upande wa kulia wa beki namba mbili ambae alionesha kuweza kuruhusu pasi za magoli matatu kutokea upande wake 
KIOJA UWANJANI 
kioja kilijitokeza pale ilipofikia hatua ya television kubwa ile ya uwanjani ilipokuwa inaonesha wachezaji wanaoanza kwenye kila timu na wale wa mapumziko,
kioja chenyewe kilianza na timu ya taifa ya Tanzania pale orodha ya wanaoanza wakiwekwa wachezaji ambao hawapo hata kwenye benchi kama vile Mrisho Ngasa na Agrey Morris
vilevile ilipofikia hatua ioneshwe timu ya ivory coast katika jina la nchi ilionesha ni timu ya taifa ya Moroco,
hii yote inaonesha jinsi gani tulivyo na maandalizi ya zima moto na kutokuwa na uweredi wa kufanya kazi kiufasaha katika vitengo tunavyopewa
RUSHWA NA USALAMA
inaonesha katika mechi hii ya leo na hata ile iliyopita siku chache ya watani wa simba na yanga usalama wake ni finyu sana kwa kuonesha polisi wao wenyewe hawazingatii kazi zao pamoja na TFF,
mfano katika mechi ya simba na yanga ilitokea polisi kuzuia watu wasiingie ndani ya uwanja kwa kusema kwamba watu wamejaa ndani na wakati watu wengi walikuwepo nje ya mageti ya uwanja wakiwa hawana tiketi,
suala hili ni kama limejirudia kwani ndani ya uwanja watu walikuwa ni wengi sana hadi wakawa wamesimama maeneo wasiyotakiwa na wengine kufikia hatua wakawa wamebanana kwenye viti vyao, kwa tukio hili linaweza kuhusishwa na rushwa inayofanya na vyombo vya dola kwa kuwaingiza watu kinyemela uwanjani bila tiketi na kutengeneza idadi kubwa ya tiketi kuliko uwezo wa uwanja.
MABOMU
muda si mrefu kama wa dakika kumi n tano polisi wa kutuliza ghasia wameweza kupiga mabomu mawili ya machozi ili kuweza kuzuia varangati lililokuwa linataka kufanywa na baadhi ya mashabiki wa taifa starz kutokana na kitendo cha kukerwa  kwa timu yetu kufungwa
kwa ujumla timu yetu ya taifa imecheza vizuri sana na tunatakiwa kuwapa pongezi kwa kiwango walichooesha na uwezo walionesha pale uwanjani, inabidi sisi watanzania tukubali kwamba kiwango chetu bado.

No comments:

Post a Comment