Azam FC yafanya kufuru Sudan Kusini, yaichakaza Al Nasri Juba 5-0
Ushindi wa 5-0 dhidi ya Al Nasri Juba ya Sudan Kusini, umeipa Azam FC
nafasi ya kuingia hatua ya pili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho
Afrika kwa kuitoa timu hiyo kwa jumla ya magoli 8-1.
Azam FC
inashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo yanayoandaliwa na
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imefanikiwa kuvuka hatua ya awali na
kuingia hatua ya pili ambapo zimesalia timu 36.
Azam FC imefikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kupata ushindi wa 3-1
katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam wiki mbili zilizopita na leo wakacheza mechi ya pili kwenye
Uwanja wa Juba nchini Sudan Kusini na kupata ushindi mnono wa 5-0 wakiwa
ugenini na kufikisha jumla ya magoli 8-1.
Kwa timu za
Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CAF, ni Azam FC pekee iliyosalia
baada ya timu za Simba SC kutolewa na Recreativo Libolo ya Angola kwa
jumla ya magoli 5-0, na Jamhuri ya Pemba nayo ikatolewa na St. George ya
Ethiopia kwa kipigo cha jumla cha 8-0 zote zilikuwa zinacheza Klabu
Bingwa Afrika.
Azam FC wanabaki kuwa wawakilishi pekee wa
Tanzania katika mashindano ya CAF, watakutana na mshindi kati ya Barrack
Y. C. II ya Liberia na Johansens ya Sierra Leone.
Katika
mchezo wa leo ambao Azam FC walipata ushindi wa 5-0, magoli yalifungwa
na Khamis Mcha magoli matatu ‘Hat Trick’, John Bocco na Salum Abubakar
wamefunga goli moja moja.
Azam Fc katika mchezo wake wa kwanza
ilipata ushindi wa 3-1 magoli ya Azam FC yakifungwa na Abdi Kassim na
Kipre Tchetche aliyefunga magoli mawili.
Kikosi kamili cha
Azam Fc kitarejea nchini kesho kwa maandalizi ya mchezo wao mwingine wa
Kombe la Shirikisho utakaochezwa kati ya Machi 15-17 mwaka huu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment