Huyu ndo ndo Bwana Mkubwa Willie Knuckles aliyekuwa waziri wa mambo
ya rais(Minister of Presidential Affairs) huko Liberia ambaye
alilazimika kujiuzulu baada ya picha zake zilizokuwa zikimwonyesha
akifanya tendo la ngono na wanawake wawili kusambazwa kwenye mtandao.
Kwakweli
bado haijaeleweka hasa walioamua kumsambaza mtandaoni walikuwa na lengo
gani naye zaidi ya kumdharirisha na kumfedhehesha namna hii.
Haijaelezwa
vizuri kuwa ndoa yake ambayo ilikuwa na takribani miaka 37 mpaka
anakutwa na maswahibu haya iliishilia vipi,vyovyote ilivyokuwa Bwana
mkubwa Knucles atakuwa alivuna alichokuwa amekipanda.
Hapa
Tanzania kina" Willie Knucles" wako wengi sana,wababa wanaopenda
kutumia nyadhifa zao na mapesa yao ambayo kwao huona ni vijisenti kwa
kuwarubuni mabinti tena wadogowadogo na kufanya nao ngono.
Binafsi
huwa nashikwa na hasira sana ninapoona binti mdogo anatoka na M'baba
anayefaa kuwa Baba yake Mzazi ni mambo ambayo yapo sana katika jamii
yetu hata kijijini kwangu ninapoishi Kiluvya wazee wa type hii wapo sana
ndo maana kasi ya kusambaa kwa virusi hatari vya Ukimwi inazidi kukua
kila kukicha,in which way tunaweza kupona ikiwa mambo haya yataachiwa
yaendelee ku'apply katika jamii zetu?
Lakini
na nyie ma'binti hivi na lazima kweli m'date na Wababa wanaolingana na
Wazazi wenu?(hili nalo ni swali ninaloliulizaga sana... majibu ambayo
nimekuwa nikiyapata yamekuwa hayaniridhishi hata kidogo,eti utamsikia
demu anasema eti Vijana wasumbufu sana....nyie mmelogwa?)
Blog
hii inatoa tahadhari,yaliyompata Bwana Willie Knucles iwe ni fundisho
kwa wote wenye tabia hii,siku hizi technolojia imekua sana,unaweza
kudhalilishwa dunia nzima katika dakika chache tu,kuna simu za kichina
siku hizi zina Camera 4,4 (mbele nyuma na pande zote 2)
Shauri zenu mnaweza kujikuta kwenye "The World of Anselm" mkabaki kunisaka kwa udi na uvumba.
No comments:
Post a Comment