http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Sunday, December 20, 2015

MSEMAJI WA TIMU YA DAR YOUNG AFRICAN KUFIKISHWA KAMATI YA MAADILI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili Msemaji wa Yanga Jerry Muro sababu ya kauli za kibaguzi dhidi Msemaji wa Simba Haji Manara.
-Muro alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari

JamiiForums's photo.
Anajiita kama siyo kujinasibu kuwa yeye ni msomi sana kwa kuwa ana master's degree ya Public Administration na kwamba ana mafanikio lukuki tu ya kimaisha.
Jana ktk press conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.
Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?

Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.
Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka ktk hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.

Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.
Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?
Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Hawa watu wenye hizi ngozi ni matatizo makubwa ndiyo maana tunawasaidia kuwalinda "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!

Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni watafuteni waandishi wa habari za michezo wawapeni uthibitisho kamili.
Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.

Binafsi nimesikitika mno!
=============================

Update

JERRY MURO KUFIKISHWA KWENYE KAMATI YA MAADILI YA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litamfikisha kwenye Kamati ya Maadlili mapema Mwakani baada ya sikukuu ya mwaka Mpya 2016, Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutokana na kauli zake za kibaguzi dhidi ya Mkuu wa Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara.

Muro alimshambulia kwa maneno ya kibaguzi Manara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika jana makao makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam.

Kauli ya Muro dhidi ya Manara ni kinyume na Katiba ya TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambao zinapiga vita vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote katika mpira wa miguu.

Mapema mwaka huu, Muro alifikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na kumshambulia na kumdhalilisha kupitia vyombo vya habari aliyekuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Fatma Abdallah. Kamati ya Nidhamu ilimwadhibu kwa kumpiga faini ya sh. milioni 5.

Chanzo:Shaffih Dauda

No comments:

Post a Comment