Timu ya Young Africans leo imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya URA kutoka nchini Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.
URA ambayo leo ilikuwa ikicheza mchezo wake wa pili baada ya jana kuibuka na ushindi wa 2-1 katika mchezo dhdi ya Simba SC iliingia uwanjan kuhakikisha inaendeleza wimbi la ushindi halli ambayo ilikua tofauti.
Watoza kodi hao kutoka nchini Uganda waliuanza mchezo kwa kasi na kupata nafasi kadhaa ya za kufunga lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango ulikua kikwazo kwao na kufanya mchezo kuchezwa zaidi eneo la katikati.
Young Africans ilikosa nafasi tatu za kujipatia mabao kupitia kwa washambuliaji wake Said Bahanuzi, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu ambao hawakuzitumia ipasavyo nafasi hizo za wazi.
Dakika ya 41 URA walijipatia bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Lutinda Yayo aliyefunga bao hilo kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Deogratius Munishi Dida na kuhesabu bao la kwanza.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Young Africans 0 - 1 URA.
Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Abdallah Mguhi aliingia kuchukua nafasi ya Shaban Kondo mabadiliko ambayo yalileta uhai na kuifanya Yanga kutawala eneo la katikikati ya uwanja.
Lutinda Yayo aliipatia tena URA bao la pili dakika ya 56 kwa mpira wa adhabu amabpo shuti lake lilijaa moja kwa moja wavuni na kufanya ubao kusomeka 2-0.
Yanga ilibadilika na kupata bao la kusawazisha dakika ya 66 ya mchezo kupitia kwa Didier Kavumbagu kwa kichwa akimalizia krosi safi iliyopigwa na mlinzi Juma Abdul aliyepanda kuongeza nguvu mashambulizi.
Watoto wa jangwani waliendelea kulishambulia lango la URA kupitia kwa washambuliaji wake lakini kutokua makini kwao kulifanya ubao wa matangazo uendelee kusomeka 2-1 huku washabiki wengine wakianza kutoka uwanjani dakika za majeruhi.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la pili na la kusawazisha dakika ya 89 ya mchezo kufuatia mpira uliopigwa na kiungo Bakari Masoud na Tegete kuwashinda ujanja walinzi wa URA na kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika,Young Africans 2 - 2 URA.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema kipindi cha kwanza wachezaji wake hawakucheza vizuri lakini kipindi cha pili walibadilika kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kusawazisha kuwa 2-2 mwisho wa mchezo.
Kesho wachezaji na benchi la ufundi watakua na mapumziko ambapo watakwenda nyumbani kwa kiungo Nizar Khalfani kumpa pole kufuatia kufiwa na baba yake mzazi jana na mazishi kufnayika leo Mbagala Kizuiani.
Timu itaendelea tena na mazoezi siku ya jumanne katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola saa 2:00 asubuhi
Young Africans: 1.Deogratius Munishi 'Dida', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Ibrahim Job, 5.Rajab Zahir, 6.Salum Telela, 7.Said Bahanuzi/Haruna Niyonzima, 8.Hamis Thabit/Bakari Masoud, 9.Jerson Tegete, 10.Didier Kavumbagu, 11.Shaban Kondo/Abdallah Mguhi 'Messi'
URA: 1.Mugali Yasin, 2.Derick Waluya, 3.Sekito Samuel, 4.Docca Musa, 5.Joseph Owino, 6.Agaba Osca, 7.Nkungwa Kinah, 8.Feni Ali, 9.Ngame Emanuel, 10.Lutinda Yayo, 11. Kasibantu James
No comments:
Post a Comment