Yanga ikicheza mchezo wake wa kwanza tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2013/2014 ilikuaa inatumia mchezo huo wa kirafiki kama maandaliz ya msimu mpya kwani mpaka sasa imeshafanikiwa kusajili wachezaji wapya watano.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts alimpanga mlinda mlango mpya langoni Deogratius Munishi 'Dida' kusimama kwenye milingoti ya lango la Yanga ambao alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya wachezaji wa KCC,
Dakika ya 40 ya mchezo kiungo mshambuliaji Hamis Thabit aliipatia timu ya Young Africans bao kwanza kwa shuti la kimo cha mbuzi liliomshinda mlinda mlango wa KCC na kuiandikia Yanga bao la kwanza.
Mpaka mapumziko Yanga ilikua mbele kwa bao 1 - 0 dhidi ya KCC.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo timu ya KCC ndio iliyonufaika na mabadiliko hayo ambapo katika dakika ya 88 ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa naodha wake Kavuma Winy aliyemalizia mpira uliozembewa kuokolewa na walinzi wa Yanga.
Mpaka mwisho wa mchezo Yanga 1 - 1 KCC.
Ziara ya Yanga kutembeza kombe la ubingwa itaendelea kesho katika mkoa wa Shinyanga kwa kucheza mwingine wa kirafiki dhidi ya timu ya KCC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Yanga: 1.Deogratius Munishi 'Dida', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Rajab Zahir, 5.Mbuyu Twite, 6.Salum Telela, 7.Nizar Khalfani/said Bahanuzi 8.Hamis Thabit/Bakari Hamadi 9.Jerson Tegete, 10.Didier Kavumbagu/Sospter, 11. Abdallah Mnguli 'Messi'/Shaban Kondo
No comments:
Post a Comment