http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/12124853/Kubenea.jpg

Tuesday, July 30, 2013

Okwi: Siendi Tunisia, Simba njooni mnichukue

 
  • Okwi, ambaye Etoile imetishia kumshitaki Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ameliambia Mwanaspoti kuwa anaidai timu hiyo fedha za usajili wake (signing fee) na amefuatilia bila mafanikio hivyo ameona ni bora akabaki Uganda hadi pale atakapokamilishiwa mzigo wote.

 straika Emmanuel Okwi jijini Kampala na ametamka kwamba hatarudi ng’o kwenye klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia mpaka imuhakikishie mambo mawili kwamba itamlipa deni lake na itamchezesha na si kumuweka benchi.
Safari hii kwa mdomo wake mwenyewe ametamka kwamba yupo tayari kurudi kuwachezea Simba au klabu nyingine muda wowote kama watafanikiwa kumalizana na Etoile na kuvunja mkataba wake huko Tunisia.
Okwi, ambaye Etoile imetishia kumshitaki Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ameliambia Mwanaspoti kuwa anaidai timu hiyo fedha za usajili wake (signing fee) na amefuatilia bila mafanikio hivyo ameona ni bora akabaki Uganda hadi pale atakapokamilishiwa mzigo wote.
“Ni kweli nawadai wale jamaa, unajua ni kwamba wakati najiunga nao walinipa fedha nusu na wakaniahidi nyingine kunipa kiasi kilichobaki ndani ya muda mfupi, lakini wamekuwa wakinizungusha tu,” alisema straika huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba.
“Nimewaambia sitarudi kwao mpaka watakaponilipa fedha zangu zilizobaki, naendesha maisha kutokana na soka sasa kama hawanilipi nifanye nini? Msimamo wangu ndio huo ni bora nibaki hapa nifanye mambo yangu,” alisisitiza mchezaji huyo ambaye hata Simba haijalipwa dau lao la kumuuza Tunisia.
“Pia sipendi vile wanavyonifanyia nilienda kule kwa ajili ya kucheza si kukaa benchi lakini tangu nimefika kule sina uhakika wa kucheza kama si kutaka kunimaliza ni nini? Niko tayari kufanya kazi na watu ambao wanataka niwafanyie kazi,” alisema Okwi.
Hata hivyo, Okwi hakutaka kutaja kiasi cha fedha anachoidai Etoile kwa madai kwamba ni siri yake.
Okwi alisema yuko tayari kwenda kucheza klabu nyingine yoyote na hata kama kurejea Simba kama itamalizana na Etoile kwani maisha ya nchini Tunisia yanaonekana kumwendea hovyo.
“Unaniuliza kama nipo tayari kurejea Simba? Ni kweli nipo tayari kabisa, kama watanihitaji mimi sina tatizo ingawa ni lazima wamalizane na wale jamaa, niliishi vizuri Dar es Salaam na naamini mashabiki bado wananipenda na wanaimani,”alisema Okwi.

No comments:

Post a Comment