Mhe. Balozi Seif Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar;
Mhe Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa;
Waheshimiwa Mawaziri; Jenerali Davis Mwamunyange, Mkuu wa Majeshi yaUlinzi;
Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi Wastaafu;Chief of Staff na Chief of Staff Wastaafu;Majenerali;
Maafisa Wakuu;
Maafisa Wadogo; Askari, Wafanyakazi raia wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa;
Waombolezaji wenzangu;
Familia za Wafiwa;
Mabibi na Mabwana.
Leo ni siku ngumu sana kutakiwa kuzungumza. Ugumuwenyewe unatokana na
ule ukweli kwamba siyo siku ya furaha bali ya majonzi na huzuni kubwa
kwangu, kwa taifaletu na familia za wanajeshi wetu saba marehemu
ambaotumekusanyika hapa kuwaaga. Baada ya sherehe zakutunuku Kamisheni
kwa Maofisa wapya katika Chuo chaMafunzo ya Kijeshi, Monduli Jumamosi
tarehe 13 Julai, 2013 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange
aliniarifukutokea shambulio la kuvizia kwa baadhi ya wanajeshi
wetuwalioko Darfur. Kwa kuwa wakati ule mapigano yalikuwayanaendelea,
aliniambia kuwa atatoa taarifa zaidi baadae kadri taarifa zitakavyokuwa
zinapatikana.
Baadae akanipa taarifa kuwa vijana wetu
wamefarikina wengine wamejeruhiwa. Lazima nikiri kuwa taarifahiyo
ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa niniwatu wa Darfur
wawaue wanajeshi wetu ambaowamekwenda kule kuwasaidia wapate utulivu,
ili kunusurumaisha yao, kuwaondolea wasiwasi na kuwawezeshawafanye
shughuli zenye tija kuendesha maisha yao. Mojakwa moja sikusita kuamini
kuwa waliofanya hivyo ni watuwahalifu.
Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea wanyongedhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na
watu wotewalioko katika mazingira hatarishi Afrika na duniani. Njia za
Kidiplomasia zilitumika na wakati mwingine JWTZlilishirikishwa. Ndio
maana tumeshiriki kwenye vita vyaukombozi katika nchi kadhaa zilizopo
Kusini mwa Afrika.Vilevile tumeshiriki katika shughuli za kulinda amani
katikanchi mbalimbali zikiwemo Liberia, Sierra Leone na Eritrea.Hivi
sasa Jeshi letu linaendelea na jukumu hilo nchiniLebanon, Cote d’Ivoire,
Darfur (Sudan), Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika nchi zote hizo,askari wetu wanasifiwa sana kwa bidii ya kazi,
uvumilivu,uhodari na nidhamu ya hali ya juu.
Wakati wote
tulipoombwa na kukubali kupelekawanajeshi wetu kutekeleza majukumu hayo,
uwezekano wawao kujeruhiwa au kufariki yanafikiriwa kutokea.Wanakwenda
kwenye maeneo yenye mapigano hivyohatari hizo kutokea ni jambo
linalowezekana. Tahadharizote husika huchukuliwa kuepusha hatari hizo.
Ndiyomaana hupewa mafunzo ya kutosha na silaha za kutosha.Hata hivyo
hutokea nyakati kukatokea yasiyotarajiwa kamayaliyotokea Darfur. Pia
yaliwahi kutokea Liberia.
Kufuatia tukio hilo, nilizungumza na
Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa ambaye alinielezea masikitiko yakemakubwa
kwa yaliyotokea na kutoa pole zake nyingi. Pia alinieleza kuwa
alizungumza na Rais Bashir wa Sudanakitaka wahalifu hao wasakwe,
wakamatwe na kuadhibiwaipasavyo. Aidha, nilifanya mazungumzo na Rais
Omar AlBashir wa Sudan, ambaye naye alinielezea masikitiko yakena kutoa
pole nyingi. Katika mazungumzo yangu naye nilimsisitizia umuhimu wa
Serikali yake kufanya uchunguziwa kina wa shambulizi hilo na
kuwawajibisha waliohusika. Rais Bashir alikubaliana nami na kuahidi
kufanya kilalinalowezekana ili ukweli ufahamike na hatua
stahikizichukuliwe.
Sisi kwa upande wetu, Jeshi la Wananchi wa
Tanzanialimeunda Bodi ya Uchunguzi inayotarajiwa kuelekea Sudankwa ajili
ya kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo chashambulizi hilo.
Kwa huko Darfur, tangu shughuli za ulinzi wa amani waUNAMID zianze
mwaka 2007 walinzi wa amani 41 kutokamataifa mbalimbali wameuawa na
zaidi ya walinzi wa amani 55 wamejeruhiwa. Kwa kweli idadi hii ni kubwa
mnoinayohitaji kutafakariwa vizuri na wadau wote. Penginewakati umefika
wa kuutazama upya mfumo wa kulindaamani Darfur hasa kuhusu uwezo wa
kujilinda na wanajeshiwanaolinda amani. Hapana budi uwezo wao uongezwe
ili kupunguza vifo na majeruhi. Narudia kuahidi kuwa rai hiitutaifikisha
kwa mamlaka husika katika Umoja wa Mataifana Umoja wa Afrika.
Napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru serikali yaSudan, Umoja wa Afrika
na Umoja wa Mataifa kwaushirikiano mkubwa waliotupatia tangu kutokea
kwa tukiola kushambuliwa kwa askari wetu. Pia nawashukuru nakutoa
pongezi kwa Waziri Shamsi Vuai Nahodha, JeneraliDavis Mwamunyange na
makamanda na askari wote wa JWTZ, kwa jinsi walivyoshughulikia msiba huu
tanguilipopokelewa taarifa ya vifo vya mashujaa wetu hawampaka sasa.
Mmewapa heshima kubwa wanaoistahili.Asanteni sana.
Kwa namna ya
pekee, narudia kutoa pole nyingi kwafamilia za wafiwa. Nawashukuru kwa
dhati kwa moyo waowa uvumilivu na subira. Naomba mfahamu kuwa, mimi
naWatanzania wote tupo pamoja nanyi katika kuombolezavifo vya mashujaa
wetu. Msiba huu ni wa taifa letu lote nawatu wote wenye kupenda amani
duniani.
Daima tutawakumbuka mashujaa wetu na tutaendeleakuenzi
na kujivunia kazi zao na mchango wao mkubwa kwanchi yetu na dunia kwa
ujumla. Nawaomba sote tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za
mashujaawetu mahala pema peponi. Amen.
Kwa Jeshi na wanajeshi
wetu wote, napenda kumaliziakwa kuwaasa kuwa yaliyotokea Darfur
yasiwakatishe tamaakatika kutimiza wajibu wetu Darfur na kwingineko.
Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
Yaliyotokeayanatukumbusha
kuchukua tahadhari zaidi na kuongezauwezo wa kujihami wa wanajeshi wetu
kila wanapotumwakutekeleza jukumu lao.
Asanteni
No comments:
Post a Comment