Wakizungumza juzi katika ofisi zetu Bamaga, Mwenge Dar kwa nyakati tofauti huku wakiomba kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya ndugu wa wanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) walio katika kazi maalum ya kulinda amani huko Darfur, DR Congo na Lebanon wamesema hofu yao inakuja baada ya kusikia kuwa huwa hawatumii silaha kujilinda.
“Sasa kama hawatumii silaha na wanatumia virungu na wenzao wanatumia bunduki tena za kisasa hofu yetu ni kwamba watazidi kushambuliwa na kuuawa,” alisema ndugu mmoja.
Ndugu mwingine alisema kwamba wanakuwa na wasiwasi mkubwa na kutaharuki kutokana na maelezo yanayotolewa kupitia vyombo vya habari vya nje kwamba Congo na Darfur mapambano hivi sasa yamepamba moto.
Moja ya jeneza lenye mwili wa mwanajeshi likiingizwa kwenye gari kwa ajili ya kusafirishwa.
“Kama mapambano yamepamba moto, hawa ndugu zetu watajihami kwa
sialaha gani? Tunaiomba serikali ifanya kila linalowezekana ili askari
wetu warudishwe nchini,” alisema jamaa mwingine aliyesema yeye kaka yake
yupo DR Congo.Majeshi hayo ya Tanzania yanalinda amani katika nchi za DR Congo, Darfur na Lebanon chini ya mkataba wa Azimio la Umoja wa Mataifa Nambari 2098 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment