Kikosi cha Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gombani kujiandaa na mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya Simba SC mchezo utakaofanyika katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi mei 18, 2013.
Kocha mkuu Ernie Brandts ameendelea kukiandaa kikosi chake kuhakikisha kinaendeleza wimbi la ushindi katika mchezo dhidi ya Simba kwani anaamini kikosi chake ni bora na ana kila sababu ya kushinda mchezo huo.
"Nina timu bora, wachezaji bora, uwezo wa wachezaji wangu ni wa hali ya juu, mshikamano na umoja katika kikosi ni wa hali ya juu, morali na mtazamo wa kila mchezaji ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo, kwa hiyo na kila sababu ya kujivunia kikosi changu kuibuka na ushindi" alisema Brandts.
Kuhusu timu ya Simba Brandts alisema wana timu nzuri lakini hiyo haimpi presha kwani kikosi cha Yanga kimekamilika kila idara, nina timu bora , nia, uwezo na sababu ya kushinda wa mchezo huo tunayo hivyo wana Yanga wakae mkao wa kushangilia Ushindi na Ubingwa siku ya jumamosi.
Aida Nahodha wa Young Africans Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kikosi kipo katika hali nzuri, wachezaji wana morali ya hali ya juu lengo ni letu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa jumamosi na kuwapa furaha wana Yanga.
Yanga iilitwaa Ubingwa ikiwa na michezo miwili mikononi kufuatia kufikisha pointi 57 ambazo hakuna timu yoyote ambayo ingeweza kufikisha idadi hiyo ya pointi kufuatia timu ya Azam FC kushindwa kuikamata Yanga na kwa kutoka sare na timu ya Coastal Union.
Huu ni Ubingwa wa 24 kwa timu ya Young Africans tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania bara ambapo watoto wa jangwani wanaongoza kwa kutwaa ubingwa huo mara nyingi kuliko timu zote nchini Tanzania.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)
No comments:
Post a Comment